Zaburi 18:17-23 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Aliniokoa kutoka kwa maadui zangu wenye nguvu nyingi,aliniokoa kutoka kwa hao walionichukia,maana walikuwa na nguvu kunishinda.

18. Walinivamia nilipokuwa taabuni,lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu.

19. Alinileta, akaniweka mahali pa usalama;alinisalimisha, kwani alipendezwa nami.

20. Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu;alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia.

21. Maana nimefuata njia za Mwenyezi-Mungu,wala sikujitenga na Mungu wangu kwa uovu.

22. Nimeshika maagizo yake yote,sikuacha kufuata masharti yake.

23. Mbele yake sikuwa na hatia;nimejikinga nisiwe na hatia.

Zaburi 18