1. Ee Mwenyezi-Mungu usikie kisa changu cha haki,usikilize kilio changu,uitegee sikio sala yangu isiyo na hila.
2. Haki yangu na ije kutoka kwako,kwani wewe wajua jambo lililo la haki.
3. Wewe wajua kabisa moyo wangu;umenijia usiku, kunichunguza,umenitia katika jaribio;hukuona uovu ndani yangu,sikutamka kitu kisichofaa.
4. Kuhusu matendo watendayo watu;mimi nimeitii amri yako,nimeepa njia ya wadhalimu.
5. Nimefuata daima njia yako;wala sijateleza kamwe.
6. Nakuita, ee Mungu, kwani wewe wanijibu;unitegee sikio, uyasikie maneno yangu.
7. Onesha fadhili zako za ajabu,uwaokoe kutoka kwa adui zao,wale wanaokimbilia usalama kwako.
8. Unilinde kama mboni ya jicho;unifiche kivulini mwa mabawa yako,