Zaburi 13:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mpaka lini ee Mwenyezi-Mungu, utanisahau?Je, utanisahau mpaka milele?Mpaka lini utanificha uso wako?

2. Nitakuwa na wasiwasi rohoni hadi lini,na sikitiko moyoni siku hata siku?Hadi lini adui zangu watafurahia taabu zangu?

3. Uniangalie na kunijibu, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu.Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo.

Zaburi 13