Zaburi 10:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Kinywa chake kimejaa laana, udanganyifu na dhuluma;mwepesi kusema maneno ya kuchukiza na maovu.

8. Hujificha vijijini huku anaotea,amuue kwa siri mtu asiye na hatia.Yuko macho kumvizia mnyonge;

9. huotea mafichoni mwake kama simba.Huvizia apate kuwakamata maskini;huwanasa kwa mtego wake na kuwachukua.

10. Mnyonge huvamiwa na kuangushwa chini;huangushwa kwa ukatili wa mtu mwovu.

11. Mwovu huwaza moyoni mwake: “Mungu amesahau;ameficha uso wake, haoni kitu!”

12. Inuka, ee Mwenyezi-Mungu, uwaadhibu;usiwasahau wanaodhulumiwa.

13. Ee Mungu, kwa nini mwovu anakudharau,na kusema ati hutamfanya awajibike?

Zaburi 10