Yohane 3:10-13 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Yesu akamjibu, “Je, wewe ni mwalimu katika Israeli na huyajui mambo haya?

11. Kweli nakuambia, sisi twasema tunayoyajua na kushuhudia tuliyoyaona, lakini nyinyi hamkubali ujumbe wetu.

12. Ikiwa nimewaambieni mambo ya kidunia nanyi hamniamini, mtawezaje kuamini nikiwaambieni mambo ya mbinguni?

13. Hakuna mtu aliyepata kwenda juu mbinguni isipokuwa Mwana wa Mtu, ambaye ameshuka kutoka mbinguni.

Yohane 3