Yohane 19:16-19 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Hapo, Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulubiwe.Basi, wakamchukua Yesu.

17. Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa” (kwa Kiebrania Golgotha).

18. Hapo ndipo walipomsulubisha, na pamoja naye waliwasulubisha watu wengine wawili; mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto, naye Yesu katikati.

19. Pilato aliandika ilani akaiweka juu ya msalaba. Nayo ilikuwa imeandikwa hivi: “Yesu Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi.”

Yohane 19