Yohane 17:14-23 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Mimi nimewapa ujumbe wako, nao ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.

15. Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naomba uwakinge na yule Mwovu.

16. Wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.

17. Waweke wakfu katika ukweli; neno lako ni ukweli.

18. Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni;

19. na kwa ajili yao mimi mwenyewe najiweka wakfu ili nao pia wafanywe wakfu katika ukweli.

20. “Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao.

21. Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.

22. Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja;

23. mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi.

Yohane 17