12. Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.
13. Basi, sasa naja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni, ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu.
14. Mimi nimewapa ujumbe wako, nao ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
15. Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naomba uwakinge na yule Mwovu.
16. Wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
17. Waweke wakfu katika ukweli; neno lako ni ukweli.
18. Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni;
19. na kwa ajili yao mimi mwenyewe najiweka wakfu ili nao pia wafanywe wakfu katika ukweli.
20. “Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao.