Yohane 11:21-28 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!

22. Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”

23. Yesu akamwambia, “Kaka yako atafufuka.”

24. Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.”

25. Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi;

26. na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?”

27. Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana! Mimi naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.”

28. Baada ya kusema hayo, Martha alikwenda kumwita Maria, dada yake, akamwambia faraghani, “Mwalimu yuko hapa, anakuita.”

Yohane 11