8. Hakuna amsukumaye mwenziwe;kila mmoja anafuata mkondo wake.Wanapita kati ya vizuizi vya silaha,wala hakuna kiwezacho kuwazuia.
9. Wanauvamia mji,wanapiga mbio ukutani;wanaziparamia nyumba na kuingia,wanapenya madirishani kama wezi.
10. Nchi inatetemeka mbele yao,mbingu zinatikisika.Jua na mwezi vyatiwa giza,nazo nyota zinaacha kuangaza.
11. Mwenyezi-Mungu anaamuru jeshi lake kwa sauti;askari wake ni wengi mno,wanaomtii hawahesabiki.2Siku ya Mwenyezi-Mungu kweli ni kuu na ya kutisha sana!Nani atakayeweza kuistahimili?
12. “Lakini hata sasa,”nasema mimi Mwenyezi-Mungu,“Nirudieni kwa moyo wote,kwa kufunga, kulia na kuomboleza.
13. Msirarue mavazi yenu kuonesha huzunibali nirudieni kwa moyo wa toba.”Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu;yeye amejaa neema na huruma;hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili;daima yu tayari kuacha kuadhibu.
14. Huenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atabadili niana kuwapeni baraka ya mazao,mkamtolea sadaka za nafaka na kinywaji.
15. Pigeni tarumbeta huko Siyoni!Toeni amri watu wafunge;itisheni mkutano wa kidini.
16. Wakusanyeni watu wote,wawekeni watu wakfu.Waleteni wazee,wakusanyeni watoto,hata watoto wanyonyao.Bwana arusi na bibi arusina watoke vyumbani mwao.