22. Je, nimesema mnipe zawadi?Au mnitolee rushwa kwa mali zenu?
23. Au mniokoe makuchani mwa adui?Au mnikomboe mkononi mwa wadhalimu?
24. “Nifundisheni, nami nitanyamaza.Nielewesheni jinsi nilivyokosea.
25. Maneno ya kweli yana nguvu kubwa!Lakini makaripio yenu yananikosoa nini?
26. Je, mnadhani kwamba mwaweza kuyakosoa maneno?Maneno ya mtu aliyekata tamaa ni upepo tu.
27. Nyinyi mnathubutu hata kuwapigia yatima kura;mnawapigia bei hata marafiki zenu!