Yobu 41:2-7 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Hakuna mtu yeyote mkali athubutuye kulishtua.Nani, basi awezaye kusimama mbele yangu?

3. Nani aliyenipa kitu, ili nitakiwe kumrudishia?Chochote kilicho chini ya mbingu ni changu.

4. “Sitaacha kukueleza juu ya viungo vya hilo dudeau juu ya nguvu zake na umbo lake zuri.

5. Nani awezaye kumbambua vazi lake la nje?Nani awezaye kutoboa deraya lililovaa?

6. Nani awezaye kufungua kinywa chake?Meno yake pande zote ni kitisho!

7. Mgongo wake umefanywa kwa safu za ngaozilizoshikamana pamoja kama kwa mhuri,

Yobu 41