Yobu 40:7-21 Biblia Habari Njema (BHN)

7. “Jikaze kama mwanamume.Nitakuuliza, nawe utanijibu.

8. Je, unataka kweli kubatilisha hukumu yangu,kuniona nina hatia ili wewe usiwe na hatia?

9. Je, una nguvu kama mimi Mungu?Waweza kunguruma kwa sauti kama yangu?

10. “Basi, jioneshe kuwa na fahari na ukuu,ujipambe kwa utukufu na fahari.

11. Wamwagie watu hasira yako kuu;mwangalie kila mwenye kiburi na kumwangusha.

12. Mwangalie kila mwenye kiburi na kumporomosha,uwakanyage waovu mahali walipo.

13. Wazike wote pamoja ardhini;mfunge kila mmoja kwa kifungo cha kifo.

14. Hapo nitakutambua,kwamba nguvu yako mwenyewe imekupa ushindi.

15. “Liangalie lile dude Behemothi,nililoliumba kama nilivyokuumba wewe.Hilo hula nyasi kama ng'ombe,

16. lakini mwilini lina nguvu ajabu,na misuli ya tumbo lake ni imara.

17. Huufanya mkia wake mgumu kama mwerezi,mishipa ya mapaja yake imeshonwa pamoja.

18. Mifupa yake ni mabomba ya shaba,viungo vyake ni kama pao za chuma.

19. “Hilo ni la kwanza la ajabu kati ya viumbe vyangu!Ni mimi Muumba wake niwezaye kulishinda.

20. Milima wanamocheza wanyama wote wa porinihutoa chakula chake.

21. Hujilaza chini ya vichaka vya miiba,na kujificha kati ya matete mabwawani.

Yobu 40