Yobu 4:6-15 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Je, kumcha Mungu si ndilo tegemeo lako?Na unyofu wako si ndilo tumaini lako?

7. Fikiri sasa: Nani asiye na hatia ambaye amepata kuangamia?Au, je, waadilifu wamepata kutupwa?

8. Nijuavyo mimi, wapandao uovu na ubaya huvuna hayohayo,

9. Mungu huwaangamiza hao kwa pumzi yake,hao huteketezwa kwa pigo la hasira yake.

10. Waovu hunguruma kama simba mkali,lakini meno yao huvunjwa.

11. Simba mwenye nguvu hufa kwa kukosa mawindo,na watoto wa simba jike hutawanywa!

12. “Siku moja, niliambiwa neno kwa siri,sikio langu lilisikia mnongono wake.

13. Nikiwa katika mawazo ya njozi za usiku,wakati usingizi mzito huwashika watu,

14. nilishikwa na hofu na kutetemeka,mifupa yangu yote ikagonganagongana.

15. Upepo ukapita mbele ya uso wangu,nywele za mwilini mwangu zikajisimamisha.

Yobu 4