18. Hata watumishi wake, Mungu hana imani nao;na malaika wake huwaona wana kosa;
19. sembuse binadamu viumbe vya udongo,watu ambao chanzo chao ni mavumbi,ambao waweza kupondwapondwa kama nondo!
20. Binadamu kwa masaa machache tu waweza kuangamia;huangamia milele bila kuacha hata alama yao!
21. Iwapo uzi unaoshikilia uhai wao ukikatwawao hufa tena bila kuwa na hekima.