Yobu 37:18-24 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Je, waweza, kuzitandaza mbingu kama yeyezikawa ngumu kama kioo cha shaba?

19. Tufundishe tutakachomwambia Mungu;maana hoja zetu si wazi, tumo gizani.

20. Je, nani anathubutu kumwambia: Nataka kuongea?Nani aseme apate balaa?

21. “Ghafla mtu hawezi tena kuona waziwazi:Jua limefichika nyuma ya mawingu,na upepo umefagia anga!

22. Mngao mzuri hutokea kaskazini;Mungu amezungukwa na utukufu wa kutisha.

23. Mungu Mwenye Nguvu asiyeweza kufikiwa na mtu,uwezo na uadilifu wake ni mkuu,amejaa wema wala hapotoshi haki kamwe.

24. Kwa hiyo, watu wote humwogopa;yeye hamjali mtu yeyote mwenye kiburi.”

Yobu 37