Yobu 36:5-16 Biblia Habari Njema (BHN)

5. “Sikiliza Mungu ni mwenye nguvuwala hamdharau mtu yeyote;uwezo wa akili yake ni mkuu mno!

6. Hawaachi waovu waendelee kuishi;lakini huwapatia wanaodhulumiwa haki zao.

7. Haachi kuwalinda watu waadilifu;huwatawaza, wakatawala na kutukuka.

8. Lakini kama watu wamefungwa minyororo,wamenaswa katika kamba za mateso,

9. Mungu huwaonesha matendo yao maovu,na kwamba wao ni watu wenye kiburi.

10. Huwafungua masikio wasikie mafunzo,na kuwaamuru warudi na kuacha uovu.

11. Wakimtii Mungu na kumtumikia,hufanikiwa katika siku zao zote;miaka yao yote huwa ya furaha.

12. Lakini wasipomtii, huangamia kwa upanga,na kufa kwa kukosa akili.

13. “Wasiomcha Mungu hupenda kukasirika,hawamlilii msaada anapowabana.

14. Hufa wangali bado vijana,maisha yao huisha kama ya walawiti.

15. Lakini Mungu huwaokoa wanyonge kwa unyonge waohutumia shida zao kuwafumbua macho.

16. Mungu alikuvuta akakutoa taabuni,akakuweka mahali pa wasaa pasipo shida,na mezani pako akakuandalia vinono.

Yobu 36