13. “Wasiomcha Mungu hupenda kukasirika,hawamlilii msaada anapowabana.
14. Hufa wangali bado vijana,maisha yao huisha kama ya walawiti.
15. Lakini Mungu huwaokoa wanyonge kwa unyonge waohutumia shida zao kuwafumbua macho.
16. Mungu alikuvuta akakutoa taabuni,akakuweka mahali pa wasaa pasipo shida,na mezani pako akakuandalia vinono.
17. “Lakini sasa umehukumiwa kama mwovu,hukumu ya haki imekukumba.
18. Jihadhari ghadhabu isije ikakufanya ukadhihaki,au ukubwa wa mali za kukukomboa ukakupotosha.
19. Je, kilio chako kitafaa kukutoa taabuni,au nguvu zako zote zitakusaidia?
20. Usitamani usiku uje,ambapo watu hufanywa watoweke walipo.
21. Jihadhari! Usiuelekee uovumaana umepatiwa mateso kukuepusha na uovu.
22. Kumbuka ukuu wa uwezo wa Mungu;nani awezaye kumfundisha kitu?
23. Nani basi aliyeweza kumpangia njia yake,au awezaye kumwambia: ‘Umekosea?’
24. “Usisahau kuyasifu matendo yake;ambayo watu wameyashangilia.