Yobu 30:4-11 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Walichuma mimea jangwani na majani msituni wakala,walikula hata mizizi ya mti wa mfagio.

5. Walifukuzwa mbali na watu,watu waliwapigia kelele kama wezi.

6. Iliwapasa kutafuta usalama mapangoni,kwenye mashimo ardhini na miambani.

7. Huko vichakani walilia kama wanyama,walikusanyika pamoja chini ya upupu.

8. Walikuwa wapumbavu wakuu na mabaradhuliambao walilazimika kufukuzwa nchini kwa kiboko.

9. “Na sasa wamenitungia wimbo wa kunizomea,nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.

10. Wananichukia na kuniepa;wakiniona tu wanatema mate.

11. Kwa kuwa Mungu amenidhoofisha na kuniaibisha,wamekuwa huru kunitendea wapendavyo.

Yobu 30