1. “Lakini sasa watu wananidhihaki,tena watu walio wadogo kuliko mimi;watu ambao baba zao niliwaona hawafaihata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.
2. Ningepata faida gani mikononi mwao,watu ambao nguvu zao zilikuwa zimewaishia?
3. Katika ufukara na njaa kaliwalitafutatafuta cha kutafuna nyikanisehemu tupu zisizokuwa na chakula.
4. Walichuma mimea jangwani na majani msituni wakala,walikula hata mizizi ya mti wa mfagio.
5. Walifukuzwa mbali na watu,watu waliwapigia kelele kama wezi.