1. Hatimaye Yobu aliamua kuongea, akailaani siku aliyozaliwa.
2. Yobu akasema:
3. “Ilaaniwe siku ile niliyozaliwa;usiku ule iliposemwa, ‘Mwana amechukuliwa mimba’
4. Siku hiyo na iwe giza!Mungu juu asijishughulishe nayo!Wala nuru yoyote isiiangaze!
5. Mauzauza na giza nene yaikumbe,mawingu mazito yaifunike.Giza la mchana liitishe!