Yobu 28:8-16 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Wanyama waendao kwa madaha hawajazikanyagawala simba hawajawahi kuzipitia.

9. Binadamu huchimbua miamba migumu kabisa,huichimbua milima na kuiondolea mbali.

10. Hupasua mifereji kati ya majabali,na jicho lake huona vito vya thamani.

11. Huziba chemchemi zisitiririke,na kufichua vitu vilivyofichika.

12. “Lakini hekima itapatikana wapi?Ni mahali gani panapopatikana maarifa?

13. Hakuna mtu ajuaye thamani ya hekima,wala hekima haipatikani nchini mwa walio hai.

14. Vilindi vyasema, ‘Hekima haimo kwetu,’na bahari yasema, ‘Haiko kwangu.’

15. Hekima haiwezi kupatikana kwa dhahabu,wala kwa kupima kiasi kingi cha fedha.

16. Haiwezi kupimwa kwa dhahabu ya Ofiri,wala kwa vito vya Sardoniki au vya rangi ya samawati,

Yobu 28