23. “Mungu aijua njia ya hekima,anajua mahali inapopatikana.
24. Maana yeye huona mpaka upeo wa dunia,huona kila kitu chini ya mbingu.
25. Alipoupa upepo uzito wake,na kuyapimia maji mipaka yake;
26. alipoamua mvua inyeshe wapi,umeme na radi vipite wapi;
27. hapo ndipo alipoiona hekima na kuitangaza,aliisimika na kuichunguza.”
28. Kisha Mungu akamwambia mwanadamu:“Tazama! Kumcha Bwana ndio hekima;na kujitenga na uovu ndio maarifa.”