Yobu 27:20-23 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Vitisho humvamia kama mafuriko;usiku hukumbwa na kimbunga.

21. Upepo wa mashariki humpeperusha akatoweka;humfagilia mbali kutoka makao yake.

22. Upepo huo humvamia bila huruma;atajaribu kuukimbia lakini mbio za bure.

23. Upepo humzomea akimbiapo,na kumfyonya toka mahali pake.

Yobu 27