1. Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu:
2. “Mungu ni mwenye uwezo mkuu,watu wote na wamche.Yeye huweka amani mpaka juu kwake mbinguni.
3. Nani awezaye kuhesabu majeshi yake?Ni nani asiyeangaziwa na mwanga wake?
4. Mtu awezaje basi, kuwa mwadilifu mbele ya Mungu?Binadamu tu awezaje kujidai kuwa safi?