1. “Mbona Mungu Mwenye Nguvu haweki wakati maalumu wa hukumu;au kwa nini wamjuao hawazijui siku hizo zake?
2. Watu wanaoondoa alama za mipaka ya mashamba,na wengine huiba mifugo na kuilisha.
3. Huwanyanganya yatima punda wao,humweka rehani ng'ombe wa mjane.
4. Huwasukuma maskini kando ya barabara;maskini wa dunia hujificha mbele yao.