Yobu 23:14-17 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Atanijulisha yote aliyonipangia;na mengi kama hayo yamo akilini mwake.

15. Hivyo, natetemeka kwa hofu mbele yake;hata nikifikiria tu napatwa na woga.

16. Mungu ameufanya moyo wangu ufifie,Mungu Mwenye Nguvu amenitia hofu.

17. Maana nimekumbwa na giza,na giza nene limetanda usoni mwangu.

Yobu 23