12. Kamwe sijaacha kushika amri yake,maneno yake nimeyatunza moyoni mwangu.
13. Lakini yeye habadiliki, nani awezaye kumgeuza?Analotaka, ndilo analofanya!
14. Atanijulisha yote aliyonipangia;na mengi kama hayo yamo akilini mwake.
15. Hivyo, natetemeka kwa hofu mbele yake;hata nikifikiria tu napatwa na woga.
16. Mungu ameufanya moyo wangu ufifie,Mungu Mwenye Nguvu amenitia hofu.
17. Maana nimekumbwa na giza,na giza nene limetanda usoni mwangu.