Yobu 22:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Umewanyima maji wale waliokuwa wamechoka;umewanyima chakula wale walio na njaa.

8. Umemruhusu mwenye cheo kuchukua ardhi yote;umemwacha anayependelewa aishi humo.

9. Umewaacha wajane waende mikono mitupu;umewanyima yatima uwezo wao.

10. Kwa hiyo mitego imekuzunguka pande zote,hofu ya ghafla imekuvamia.

11. Giza limekuangukia usione kitu;mafuriko ya maji yamekufunika.

12. Twajua Mungu yuko huko juu mbinguni.Tazama nyota za juu kabisa zilivyo mbali!

13. Lakini wewe wasema: ‘Mungu ajua nini?Je, aweza kupenya mawingu akatoa hukumu?

Yobu 22