5. La! Uovu wako ni mkubwa mno!Ubaya wako hauna mwisho!
6. Wewe umemnyanganya ndugu yako nguo ya rehani;umemchukulia nguo hiyo moja aliyokuwa nayo.
7. Umewanyima maji wale waliokuwa wamechoka;umewanyima chakula wale walio na njaa.
8. Umemruhusu mwenye cheo kuchukua ardhi yote;umemwacha anayependelewa aishi humo.