24. ukitupilia mbali mali yako,ukaitupa dhahabu ya Ofiri ukingoni mwa kijito,
25. Mungu Mwenye Nguvu akawa ndio dhahabu yako,na fedha yako ya thamani;
26. basi, ndipo utakapomfurahia Mungu mwenye nguvuna kutazama kwa matumaini;
27. utamwomba naye atakusikiliza,nawe utazitimiza nadhiri zako.
28. Chochote utakachoamua kitafanikiwa,na mwanga utaziangazia njia zako.
29. Maana, Mungu huwaporomosha wenye majivuno,lakini huwaokoa wanyenyekevu.
30. Yeye humwokoa mtu asiye na hatia;wewe utaokolewa kwa matendo yako mema.”