13. Lakini wewe wasema: ‘Mungu ajua nini?Je, aweza kupenya mawingu akatoa hukumu?
14. Mawingu mazito yamemzunguka asipate kuonayeye hutembea nje ya anga la dunia!’
15. “Je, umeamua kufuata njia za zamaniambazo watu waovu wamezifuata?
16. Hao walifagiliwa kabla ya wakati wao,misingi yao ilikumbwa mbali na maji.
17. Hao ndio waliomwambia Mungu, ‘Achana nasi!’Na ‘Wewe Mungu Mwenye Nguvu waweza nini juu yetu?’
18. Lakini Mungu ndiye aliyejaza nyumba zao fanaka,lakini walimweka mbali na mipango yao!