Yobu 20:5-9 Biblia Habari Njema (BHN)

5. mwovu atajiona ameshinda kwa muda tu,furaha yake asiyemcha Mungu ni ya muda mfupi tu!

6. Mwovu aweza kufana hata kufikia mbingu,kichwa chake kikafika kwenye mawingu,

7. lakini atatupiliwa mbali kama mavi yake.Waliopata kumjua watajiuliza: ‘Yuko wapi?’

8. Atatoweka kama ndoto, asionekane tena,atafutika kama maono ya usiku.

9. Aliyemwona, hatamwona tena,wala pale alipoishi hapatatambuliwa tena.

Yobu 20