Yobu 19:9-17 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Amenivua fahari yangu;ameiondoa taji yangu kichwani.

10. Amenivunja pande zote, nami nimekwisha;tumaini langu amelingoa kama mti.

11. Ameichochea ghadhabu yake dhidi yangu;ameniona kuwa kama adui yake.

12. Majeshi yake yanijia kwa pamoja;yametengeneza njia ya kuja kwangu,yamepiga kambi kuizunguka nyumba yangu.

13. Mungu amewaweka ndugu zangu mbali nami;rafiki zangu wakuu wamenitoroka kabisa.

14. Jamaa zangu na marafiki hawanisaidii tena.

15. Wageni nyumbani mwangu wamenisahau;watumishi wangu wa kike waniona kuwa mgeni.Mimi nimekuwa kwao mtu wasiyemjua.

16. Namwita mtumishi wangu lakini haitikii,ninalazimika kumsihi sana kwa maneno.

17. Nimekuwa kinyaa kwa mke wangu;chukizo kwa ndugu zangu mwenyewe.

Yobu 19