Yobu 19:5-15 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mnaishusha hadhi yangu mpate kujikuza;mnanilaumu kwa kunyenyekezwa kwangu.

6. Jueni kwamba Mungu amenitendea vibaya,na kuninasa katika wavu wake.

7. Tazama napiga yowe: ‘Dhuluma!’Lakini sijibiwi.Naita kwa sauti kubwa,lakini sipati haki yangu.

8. Njia yangu ameiziba kwa ukuta ili nisipiteamezitia giza njia zangu.

9. Amenivua fahari yangu;ameiondoa taji yangu kichwani.

10. Amenivunja pande zote, nami nimekwisha;tumaini langu amelingoa kama mti.

11. Ameichochea ghadhabu yake dhidi yangu;ameniona kuwa kama adui yake.

12. Majeshi yake yanijia kwa pamoja;yametengeneza njia ya kuja kwangu,yamepiga kambi kuizunguka nyumba yangu.

13. Mungu amewaweka ndugu zangu mbali nami;rafiki zangu wakuu wamenitoroka kabisa.

14. Jamaa zangu na marafiki hawanisaidii tena.

15. Wageni nyumbani mwangu wamenisahau;watumishi wangu wa kike waniona kuwa mgeni.Mimi nimekuwa kwao mtu wasiyemjua.

Yobu 19