Yobu 19:15-29 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Wageni nyumbani mwangu wamenisahau;watumishi wangu wa kike waniona kuwa mgeni.Mimi nimekuwa kwao mtu wasiyemjua.

16. Namwita mtumishi wangu lakini haitikii,ninalazimika kumsihi sana kwa maneno.

17. Nimekuwa kinyaa kwa mke wangu;chukizo kwa ndugu zangu mwenyewe.

18. Hata watoto wadogo hunidharau,mara ninapojitokeza wao hunizomea.

19. “Rafiki zangu wakuu wanachukizwa nami,wale niliokuwa nikiwapenda wamenipa kisogo.

20. Mwili wangu umebakia tu mifupa na ngozi,nimeponea chupuchupu baada ya kupoteza yote.

21. Nioneeni huruma,nioneeni huruma enyi rafiki zangu;maana mkono wa Mungu umenifinya.

22. Kwa nini mnanifuatia kama Mungu?Mbona hamtosheki na mwili wangu?

23. “Laiti maneno yangu yangeandikwa!Laiti yangeandikwa kitabuni!

24. Laiti yangechorwa kwa chuma na risasijuu ya jiwe ili yadumu!

25. Najua wazi Mkombozi wangu anaishi,mwishowe yeye atanipa haki yangu hapahapa duniani.

26. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivyo,nitamwona Mungu kwa macho yangu mwenyewe.

27. Mimi mwenyewe nitakutana naye;mimi mwenyewe na si mwingine nitamwona kwa macho.

28. “Nyinyi mwaweza kujisemea:‘Tutamfuatia namna gani?

29. Tutapataje kwake kisa cha kumshtaki?’Lakini tahadharini na adhabu.Chuki yenu yaweza kuwaletea kifo!Mnapaswa kujua: Mungu peke yake ndiye hakimu.”

Yobu 19