Yobu 18:2-14 Biblia Habari Njema (BHN)

2. “Utawinda maneno ya kusema hadi lini?Tafakari vizuri nasi tutasema.

3. Kwa nini unatufanya kama ng'ombe?Mbona unatuona sisi kuwa wapumbavu?

4. Wewe unajirarua mwenyewe kwa hasira zako.Kwani, dunia itaachwa tupu kwa ajili yakoau miamba ihamishwe toka mahali pake?

5. “Naam, mwanga wa mtu mwovu utazimishwa;mwali wa moto wake hautangaa.

6. Nyumbani kwake mwanga ni giza,taa inayomwangazia itazimwa.

7. Hatua zake ndefu zitafupishwa;mipango yake itamwangusha chini.

8. Nyayo zake mwenyewe zitamtia mtegoni;kila akitembea anakumbana na shimo.

9. Mtego humkamata kisiginoni,tanzi humbana kabisa.

10. Amefichiwa kitanzi ardhini;ametegewa mtego njiani mwake.

11. Hofu kuu humtisha kila upande,humfuata katika kila hatua yake.

12. Alikuwa na nguvu, lakini sasa njaa imembana;maafa yako tayari kumwangusha.

13. “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake,maradhi ya kifo hula viungo vyake.

14. Anangolewa katika nyumba aliyoitegemea,na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.

Yobu 18