Yobu 18:10-21 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Amefichiwa kitanzi ardhini;ametegewa mtego njiani mwake.

11. Hofu kuu humtisha kila upande,humfuata katika kila hatua yake.

12. Alikuwa na nguvu, lakini sasa njaa imembana;maafa yako tayari kumwangusha.

13. “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake,maradhi ya kifo hula viungo vyake.

14. Anangolewa katika nyumba aliyoitegemea,na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.

15. Nyumba yake tupu, wengine wataishi humo;madini ya kiberiti yametawanywa katika makao yake.

16. Yeye ni kama mti uliokauka mizizi,matawi yake juu yamenyauka.

17. Nchini hakuna atakayemkumbuka;jina lake halitatamkwa tena barabarani.

18. Ameondolewa mwangani akatupwa gizani;amefukuzwa mbali kutoka duniani.

19. Hana watoto wala wajukuu;hakuna aliyesalia katika makao yake.

20. Watu wa magharibi wameshangazwa na yaliyompata,hofu imewakumba watu wa mashariki.

21. Hayo ndio yanayowapata wasiomjali Mungu;hapo ndipo mahali pa wasiomjua Mungu.”

Yobu 18