Yobu 13:9-23 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Je, akiwakagua nyinyi mtapona?Au mnadhani mnaweza kumdanganya Mungu kama watu?

10. Hakika yeye atawakemeakama mkionesha upendeleo kwa siri.

11. Je, fahari yake haiwatishi?Je, hampatwi na hofu juu yake?

12. Misemo yenu ni methali za majivu,hoja zenu ni ngome za udongo.

13. “Nyamazeni, nami niongee.Yanipate yatakayonipata.

14. Niko tayari hata kuhatarishamaisha yangu;

15. Mungu aniue akitaka, sina la kupoteza,hata hivyo nitautetea mwenendo wangu mbele yake.

16. Kama nikifaulu hapo nitakuwa nimeshinda,maana mtu mwovu hawezi kwenda mbele yake.

17. Sikilizeni kwa makini maneno yangu,maelezo yangu na yatue masikioni mwenu.

18. Kesi yangu nimeiandaa vilivyo,nina hakika mimi sina hatia.

19. “Nani atakayeipinga hoja yangu?Niko tayari kunyamaza na kufa.

20. Mungu wangu, nijalie tu haya mawili,nami sitajificha mbali na wewe:

21. Kwanza uniondolee mkono wako unaonipiga,na usiniangamize kwa kitisho chako.

22. “Uanze kutoa hoja yako nami nikujibu.Au mimi nianze, nawe unijibu.

23. Makosa na dhambi zangu ni ngapi?Nijulishe hatia na dhambi yangu.

Yobu 13