Yobu 13:2-21 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Yote mnayoyajua, mimi pia nayajua.Mimi si mtu duni kuliko nyinyi.

3. Lakini ningependa kusema na Mungu mwenye nguvu,natamani kujitetea mbele zake Mungu.

4. Lakini nyinyi mnaupakaa uongo chokaa;nyinyi nyote ni waganga wasiofaa kitu.

5. Laiti mngekaa kimya kabisa,ikafikiriwa kwamba mna hekima!

6. Sikilizeni basi hoja yangu,nisikilizeni ninapojitetea.

7. Je, mnadhani mwamtumikia Mungu kwa kusema uongo?Mnafikiri kusema kwa hila kunamfaa yeye?

8. Je, mnajaribu kumpendelea Mungu?Je, mtamtetea Mungu mahakamani?

9. Je, akiwakagua nyinyi mtapona?Au mnadhani mnaweza kumdanganya Mungu kama watu?

10. Hakika yeye atawakemeakama mkionesha upendeleo kwa siri.

11. Je, fahari yake haiwatishi?Je, hampatwi na hofu juu yake?

12. Misemo yenu ni methali za majivu,hoja zenu ni ngome za udongo.

13. “Nyamazeni, nami niongee.Yanipate yatakayonipata.

14. Niko tayari hata kuhatarishamaisha yangu;

15. Mungu aniue akitaka, sina la kupoteza,hata hivyo nitautetea mwenendo wangu mbele yake.

16. Kama nikifaulu hapo nitakuwa nimeshinda,maana mtu mwovu hawezi kwenda mbele yake.

17. Sikilizeni kwa makini maneno yangu,maelezo yangu na yatue masikioni mwenu.

18. Kesi yangu nimeiandaa vilivyo,nina hakika mimi sina hatia.

19. “Nani atakayeipinga hoja yangu?Niko tayari kunyamaza na kufa.

20. Mungu wangu, nijalie tu haya mawili,nami sitajificha mbali na wewe:

21. Kwanza uniondolee mkono wako unaonipiga,na usiniangamize kwa kitisho chako.

Yobu 13