Yobu 11:5-9 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Laiti Mungu angefungua kinywa chakeakatoa sauti yake kukujibu!

6. Angekueleza siri za hekima,maana yeye ni mwingi wa maarifa.Jua kwamba Mungu hakuhesabu makosa yako yote.

7. “Je, unaweza kugundua siri zake Munguna kujua ukomo wake yeye Mungu mwenye nguvu?

8. Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini?Kimo chake chapita Kuzimu,wewe waweza kujua nini?

9. Ukuu huo wapita marefu ya dunia,wapita mapana ya bahari.

Yobu 11