Yobu 11:16-20 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Utazisahau taabu zako zote;utazikumbuka tu kama mafuriko yaliyopita.

17. Maisha yako yatangaa kuliko jua la adhuhuri,giza lake litabadilika kuwa mngao wa pambazuko.

18. Utakuwa na ujasiri maana lipo tumaini;utalindwa na kupumzika salama.

19. Utalala bila kuogopeshwa na mtu;watu wengi watakuomba msaada.

20. Lakini waovu macho yao yatafifia,njia zote za kutorokea zitawapotea;tumaini lao la mwisho ni kukata roho!”

Yobu 11