13. “Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu,utainua mikono yako kumwomba Mungu!
14. Kama una uovu, utupilie mbali.Usikubali ubaya uwemo nyumbani mwako.
15. Hapo utajitokeza mbele ya watu bila lawama,utakuwa thabiti bila kuwa na hofu.
16. Utazisahau taabu zako zote;utazikumbuka tu kama mafuriko yaliyopita.
17. Maisha yako yatangaa kuliko jua la adhuhuri,giza lake litabadilika kuwa mngao wa pambazuko.
18. Utakuwa na ujasiri maana lipo tumaini;utalindwa na kupumzika salama.
19. Utalala bila kuogopeshwa na mtu;watu wengi watakuomba msaada.