Yobu 10:2-10 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Nitamwambia Mungu: Usinihukumu.Nijulishe kisa cha kupingana nami.

3. Je, ni sawa kwako kunionea,kuidharau kazi ya mikono yakona kuipendelea mipango ya waovu?

4. Je, una macho kama ya binadamu?Je, waona kama binadamu aonavyo?

5. Je, siku zako ni kama za binadamu?Au miaka yako kama ya binadamu,

6. hata uuchunguze uovu wangu,na kuitafuta dhambi yangu?

7. Wewe wajua kwamba mimi sina hatia,na hakuna wa kuniokoa mikononi mwako.

8. Mikono yako iliniunda na kuniumba,lakini sasa wageuka kuniangamiza.

9. Kumbuka kwamba uliniumba kwa udongo.Je, utanirudisha tena mavumbini?

10. Je, si wewe uliyenimimina kama maziwa,na kunigandisha kama jibini?

Yobu 10