Yobu 10:19-22 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Ningepelekwa moja kwa moja kaburini,nikawa kama mtu asiyepata kuwako.

20. Je, siku za maisha yangu si chache?Niachie nipate faraja kidogo,

21. kabla ya kwenda huko ambako sitarudi,huko kwenye nchi ya huzuni na giza nene;

22. nchi ya huzuni na fujo,ambako mwanga wake ni kama giza.”

Yobu 10