Yeremia 51:34-42 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Mfalme Nebukadneza wa Babulonialiuharibu na kuuponda mji wa Yerusalemualiuacha kama chungu kitupu;aliumeza kama joka.Alijaza tumbo lake vitu vyake vizurivizuri,akautupilia mbali kama matapishi.

35. Watu wa Yerusalemu na waseme:“Babuloni na ulipizwe ukatili uleule,tuliotendwa sisi pamoja na jamaa zetu!Babuloni ipatilizwekwa umwagaji wa damu yetu.”

36. Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu:“Nitawatetea kuhusu kisa chenu,na kulipiza kisasi kwa ajili yenu.Nitaikausha bahari ya Babulonina kuvifanya visima vyake vikauke.

37. Babuloni itakuwa rundo la magofu,itakuwa makao ya mbweha,itakuwa kinyaa na kitu cha kuzomewa;hakuna mtu atakayekaa huko.

38. Wababuloni watanguruma pamoja kama simba;watakoroma kama wanasimba.

39. Wakiwa na uchu mkubwanitawaandalia karamu:Nitawalewesha mpaka wapepesuke;nao watalala usingizi wa daimana hawataamka tena.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

40. Nitawashusha chini kama kondoo wa kuchinjwa,kama vile kondoo dume na beberu.

41. Ajabu kutekwa kwa Babuloni;mji uliosifika duniani kote umechukuliwa!Babuloni umekuwa kinyaa kati ya mataifa!

42. Bahari imefurika juu ya Babuloni,Babuloni imefunikwa mawimbi yaliyochafuka.

Yeremia 51