Yeremia 45:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Haya ndiyo maneno aliyotamka nabii Yeremia mnamo mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia naye Baruku mwana wa Neria akawa anayaandika kitabuni.Yeremia alimwambia Baruku:

2. “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi juu yako wewe Baruku:

3. Wewe ulisema, ‘Ole wangu! Mwenyezi-Mungu ameniongezea uchungu juu ya maumivu yangu. Nimechoka kupiga kite, wala sipati pumziko.’

4. Lakini Mwenyezi-Mungu ameniambia nikuambie hivi: Tazama, yale niliyojenga nayabomoa, na yale niliyopanda nayangoa; nitafanya hivyo katika nchi yote.

Yeremia 45