Yeremia 44:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi waliokuwa wanakaa nchini Misri katika miji ya Migdoli, Tahpanesi, Memfisi na sehemu ya Pathrosi:

2. “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi: Nyinyi mmeona maafa yote niliyouletea mji wa Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Miji hii ni magofu mpaka leo wala hakuna mtu aishiye humo.

3. Imekuwa hivyo kwa sababu ya uovu walioufanya, wakanikasirisha kwa kuifukizia ubani na kuitumikia miungu mingine ambayo wao wenyewe hawakuifahamu, wala nyinyi, wala wazee wenu.

Yeremia 44