1. Yeremia alipomaliza kuwaambia watu wote maneno yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, alimwamuru awatangazie,
2. Azaria mwana wa Hoshaia, Yohanani mwana wa Karea na watu wote mafidhuli, walimwambia Yeremia: “Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, hakukutuma wewe utuambie tusiende Misri, tukaishi huko.
3. Baruku mwana wa Neria, amekuchochea dhidi yetu ili tutiwe mikononi mwa Wakaldayo watuue au watupeleke uhamishoni Babuloni.”
4. Basi, Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote hawakutii aliyosema Mwenyezi-Mungu, kwamba wabaki katika nchi ya Yuda.