Yeremia 21:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hili ni neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu, wakati mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkia, na kuhani Sefania mwana wa Maaseya, wamwambie Yeremia hivi:

2. “Tafadhali, tuombee kwa Mwenyezi-Mungu maana Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, anaanza vita dhidi yetu. Labda Mwenyezi-Mungu atatufanyia mwujiza kama afanyavyo mara kwa mara na kumfanya Nebukadneza atuache na kwenda zake.”

3. Yeremia akawaambia:

4. Nendeni mkamwambie Sedekia kwamba hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli: “Sedekia! Nitakugeuzia wewe mwenyewe silaha unazotumia kupigana na mfalme wa Babuloni na Wakaldayo wanaowazingira nje ya kuta za mji. Nitazikusanya silaha zote katikati ya mji huu.

5. Mimi mwenyewe nitapigana nawe kwa mkono ulionyoka na wenye nguvu, kwa hasira, ukali na ghadhabu kubwa.

6. Nitawaua wakazi wa mji huu: Binadamu na wanyama kadhalika. Watakufa kwa maradhi mabaya sana.

Yeremia 21